Muswada wa Mabadiliko ya Sheria ya Idara ya Usalama wa Taifa unaoifanya iwe chini ya Usimamizi wa Rais watua Bungeni.

Kupitia Bunge la 12 linaloendelea Jijini Dodoma, Serikali imepeleka Bungeni Muswada unaopendeleza Mabadiliko ya Sheria ya Idara ya Usalama wa Taifa.

Pamoja na Mambo mengine, Sheria inapendekezwa kufanyiwa marekebisho katika kifungu cha 13 ili kuweka utaratibu wa kuapishwa kwa Mkurugenzi Mkuu, Naibu Wakurugenzi Wakuu, Wakurugenzi na Maafisa wa Idara.

Inapendekezwa kifungu cha 16 kifanyiwe marekebisho ili kuzuia ufichuaji wa utambulisho wa watu wanaofanya kazi katika Idara au watu wengine wanaoshirikiana na Idara na kumpa Mkurugenzi Mkuu mamlaka ya udhibiti wa watu hao. Lengo la marekebisho ni kuwalinda maafisa na watu hao kutokana na utendaii wao wa kazi za kiusalama.

Kifungu cha 19 kinapendekezwa kurekebishwa ili kuongeza kinga ya makosa ya jinai kwa Maafisa wa Idara tofauti na ilivyo sasa ambapo kinga imetolewa katika mashauri ya madai pekee dhidi ya Maafisa hao.

Lengo la marekebisho ni kuweka kinga dhidi ya makosa yanayoweza kutendeka wakati wa utekelezaji wa majukumu yao kwa uaminifu.

Vifungu vya 16(3), 17(3), 20(2) na 23 vinapendekezwa kurekebishwa ili kuongeza viwango vya adhabu kwa makosa mbalimbali kutegemeana na uzito wa kosa. Lengo la marekebisho hayo ni kuhakikisha viwango hivyo vya adhabu vinaendana na mazingira ya sasa.

Muswada unapendekezwa kuongeza vifungu vipya vya 24, 25 na 26 vitakavyoweka masharti mbalimbali ikiwemo, udhibiti wa Maafisa kutoa taarifa pindi wanapostaafu au kumaliza vipindi vya ajira, kuzuia uingiaji katika maeneo ya Idara bila idhini na masharti kuhusu vitendo vya uvunjifu wa Sheria nje ya mipaka ya Nchi.

Inapendekezwa Jedwali lifanyiwe marekebisho kwa kuongeza kiapo cha Utii pamoja na kurekebisha kiapo cha utumishi na kiapo cha kutunza siri kwa lengo la kumarisha ulinzi wa taarifa na ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya Idara.

Muswada huu unapendekeza kufanya marekebisho katika Sheria ya Idara ya Usalama wa Taifa, Sura ya 406. Lengo la marekebisho yanayopendekezwa ni kubadili masharti ya Sheria kuendana na mfumo wa utawala uliopo na taratibu za usimamizi wa Idara za Usalama kimataifa na kuweka masharti mbalimbali ya utekelezaji bora wa majukumu ya Idara.

Marekebisho yanakusudia kuboresha Sheria na kutatua changamoto mbalimbali zilizojitokeza wakati wa utekelezaji wake.

Muswada umegawanyika katika Sehemu Mbili. Sehemu ya Kwanza inahusu masharti ya awali ambayo yanajumuisha jina la Muswada na masharti kuhusu namna ambavyo vifungu mbalimbali vya Sheria
vimefanyiwa marekebisho.

Sehemu ya Pili ya Muswada inapendekeza marekebisho katika vifungu mbalimbali vya Sheria. Sheria inapendekeza kurekebishwa kwa ujumla kwa kubadili masharti yote kuhusu usimamizi wa Idara kutoka kwa Waziri mwenye dhamana na masuala ya Usalama wa Taifa na kuweka jukumu hilo kwa Rais.

Lengo la mapendekezo hayo ni kukidhi muundo uliopo sasa ambapo Idara ya Usalama wa Taifa inawajibika moja kwa moja kwa Rais pasipo kupitia kwa Waziri mwenye dhamana na masuala ya Usalama wa Taifa. Mapendekezo haya yamezingatia pia mfumo wa utendaji kazi wa idara za usalama duniani.

Kufuatia mabadiliko ya jumla yanayoweka usimamizi wa Idara chini ya Rais, inapendekezwa vifungu vya 11, 15, 18, 19(3) virekebishwe ili kuondoa mamlaka ya usimamizi wa Waziri wa Mambo ya Nje, Katibu Mkuu Kiongozi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika masuala mbalimbali yanayohusu usimamizi wa intelijensia na usalama.

Inapendekezwa kifungu cha 4 cha Sheria kifanyiwe marekebisho kwa kuipa Idara hadhi ya Chombo cha Ulinzi na Usalama na kuiweka chini ya usimamizi wa Rais. Lengo la marekebisho hayo ni kutambua jukumu ambalo Idara imekuwa ikitekeleza kama mojawapo ya Vyombo vya Ulinzi na Usalama Nchini.

Inapendekezwa sheria ifanyiwe marekebisho katika kifungu cha 5 kwa lengo la kuipa Idara majukumu ya msingi na muhimu ya usalama inayoyatekeleza kwa sasa. Majukumu hayo ni pamoja na ulinzi binafsi wa Viongozi wa Ngazi za Juu wa Kitaifa na Kimataifa, ulinzi wa Vituo Muhimu, mamlaka ya upekuzi wa kiusalama wa Viongozi na udhibiti wa matishio ya kiusalama dhidi ya Jamhuri ya Muungano.

Kifungu kipya cha 5A kinapendekezwa kuongezwa ili kujumuisha wajibu wa Waziri katika Sheria. Lengo la marekebisho haya ni kuwezesha masuala ya kisera ya Idara yanayotekelezwa na Waziri.

Inapendekeza kifungu cha 6 cha Sheria kifanyiwe marekebisho ili kuweka sifa za uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu na kuweka masharti kuhusu nafasi hiyo baada ya utumishi. Lengo ni kupata mtendaji mwenye uwezo, sifa na weledi na kulinda maslahi ya kiusalama kwa watu ambao wamewahi kutumikia nafasi ya Mkurugenzi Mkuu.

Ili kuboresha utendaji kazi wa Idara, inapendekezwa kuongeza vifungu 6A na 6B katika Sheria ili kuweka masharti kuhusu nafasi za Naibu Wakurugenzi Wakuu kwa Tanzania Bara na Zanzibar pamoja na nafasi ya Wakurugenzi wengine katika Idara watakaoteuliwa na Rais. Pia inapendekezwa kuweka masharti kuhusu sifa za uteuzi katika nafasi hizo tajwa.

Ili kuboresha utendaji kazi wa Idara, inapendekezwa kifungu cha 7 cha Sheria kirekebishwe kwa kuweka masharti kuhusu vigezo vya ajira kwa Watumishi wa Idara. Vilevile, kifungu kinaweka sharti la matumizi ya silaha wakati wa utekelezaji wa majukumu yao kwa lengo la kutambua matumizi ya silaha na kuweka utaratibu wa nidhamu ya umiliki na matumizi ya silaha hizo.

Inapendekezwa Kifungu cha 10 cha Sheria kifanyiwe marekebisho ili kumtambua Mkurugenzi Mkuu kama Mshauri Mkuu wa Rais na Serikali katika masuala ya usalama wa Taifa. Lengo ni kutambua wajibu wa Idara katika usimamizi na udhibiti wa Usalama wa Taifa. Vilevile, kwa kuwa Mkurugenzi Mkuu ndiye Mtendaji Mkuu wa Idara, Sheria inarekebishwa kwa kumpa Mkurugenzi Mkuu mamlaka ya nidhamu kwa watumishi walio chini yake.

Kifungu cha 10A kinapendekezwa kuongezwa ili kuweka masharti yatakayo muwezesha Katibu Mkuu Kiongozi kuratibu na kuwa kiungo baina ya Rais na Idara katika utekelezaji wa masuala ya kisera na utumishi wa umma.

Sheria inapendekezwa kufanyiwa marekebisho katika kifungu cha 13 ili kuweka utaratibu wa kuapishwa kwa Mkurugenzi Mkuu, Naibu Wakurugenzi Wakuu, Wakurugenzi na Maafisa wa Idara.

Inapendekezwa kifungu cha 16 kifanyiwe marekebisho ili kuzuia ufichuaji wa utambulisho wa watu wanaofanya kazi katika Idara au watu wengine wanaoshirikiana na Idara na kumpa Mkurugenzi Mkuu mamlaka ya udhibiti wa watu hao. Lengo la marekebisho ni kuwalinda maafisa na watu hao kutokana na utendaji wao wa kazi za kiusalama.

Kifungu cha 19 kinapendekezwa kurekebishwa ili kuongeza kinga ya makosa ya jinai kwa Maafisa wa Idara tofauti na ilivyo sasa ambapo kinga imetolewa katika mashauri ya madai pekee dhidi ya Maafisa hao.

Lengo la marekebisho ni kuweka kinga dhidi ya makosa yanayoweza kutendeka wakati wa utekelezaji wa majukumu yao kwa uaminifu.

Vifungu vya 16(3), 17(3), 20(2) na 23 vinapendekezwa kurekebishwa ili kuongeza viwango vya adhabu kwa makosa mbalimbali kutegemeana na uzito wa kosa. Lengo la marekebisho hayo ni kuhakikisha viwango hivyo vya adhabu vinaendana na mazingira ya sasa. Muswada unapendekezwa kuongeza vifungu vipya vya 24, 25 na 26 vitakavyoweka masharti mbalimbali ikiwemo, udhibiti wa Maafisa kutoa taarifa pindi wanapostaafu au kumaliza vipindi vya ajira, kuzuia uingiaji katika maeneo ya Idara bila idhini na masharti kuhusu vitendo vya uvunjifu wa Sheria nje ya mipaka ya Nchi.

Inapendekezwa Jedwali lifanyiwe marekebisho kwa kuongeza kiapo cha Utii pamoja na kurekebisha kiapo cha utumishi na kiapo cha kutunza siri kwa lengo la kuimarisha ulinzi wa taarifa na ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya Idara.

Maoni ya Wadau mbalimbali kuhusiana na muswada huu:

Zitto Kabwe

Kiongozi wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe akizungumza katika mkutano wa hadhara Ktavi, amesema;


"Tulivyopata taarifa kuwa muswada wa sheria ya usalama wa Taifa umefichwa - fichwa tukasema, wametusikia na sasa wameuweka wazi kwamba sasa wataujadili.Hii ndiyo faida ya vyama vingi kwamba tunasema,wanasikia,wanaona kuwa wamekosea na baadae wanasahihisha.


"Muswada wa sheria ya usalama wa Taifa una baadhi ya maeneo mazuri sana ambapo kwa asilimia 60 unaboresha idara ya usalama, inarasimisha idara, inaboresha maeneo ambayo ni ya kizamani na sasa yanaenda kuwa ya kisasa.


"Asilimia 40 ya Muswada wa sheria ya usalama wa Taifa ina matatizo,ambapo kuna masuala ya haki za watu yanaenda kukandamizwa na sisi ACT wito wetu ni kutaka mabovu yaboreshwe na hakuna haja ya kuharakisha sheria hii.


"Muswada huu wa sheria ya usalama wa Taifa kama utapita hivi ulivyo, unaenda kutoa kinga ya kijinai kwa Maafisa wa usalama kwamba akifanya makosa ya kijinai kwenye majukumu yake ya kikazi haitowezekana kumshtaki."




"Maafisa usalama wa Taifa (TISS) ndiyo wanalaumiwa kwa utekaji wa watu, ndiyo wanaovuruga uchaguzi, ndiyo wanaotishia watu mtaani. Ukiwaruhusu hawa watu wateke halafu ikibainika wameteka sheria inazuia kumpeleka mahakamani, watateka zaidi.


"Kipindi ambacho sheria haiwapi kinga wameteka! vipi wakiwa na kinga? Sasa hivi tuna Rais Samia ndiyo ila atamaliza muda wake. Nani kasema CCM haina Magufuli mwingine? Wanao, wanawatoa tu kabatini baada ya kusoma upepo wa kisiasa unavyoenda.


Sheria ya usalama wa taifa ya Marekani imewapa kinga CIA, Uingereza imewapa kinga maafisa wao wa idara za MI5 na MI6.Wenzetu wanachokifanya kwa maafisa wao ni kwamba ukiitumia kinga yako vibaya inaweza kuondolewa na ukafikishwa mahakamani.


"Kwenye muswada wa sheria yetu lazima tuwe na kifungu kitakacholazimisha uwepo wa kamati ya kibunge ya kusimamia idara ya usalama wa Taifa ambayo inaweza kuondoa kinga kwa afisa wa TISS, ili kuruhusu kuchunguzwa pale wanapovunja haki za binadamu kwenye majukumu yao.


"Wakati wa mjadala Bunge likiridhia kuundwa kwa Kamati ya kuisimamia idara ya TISS kwenye muswada huu, kamati itakayoundwa ijumuishe pia wabunge wa upinzani. Bunge kamili linakuja baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2025,sio bunge hili la sasa.


"Lazima pia mabadiliko haya ya sheria ya usalama wa taifa yaweke udhibiti wa matumizi mabaya ya ofisi kwa maafisa wa usalama wa Taifa (TISS), bila kufanya hivyo na wakafanikiwa kuwa na kinga ya kutoshtakiwa wataua na kutesa sana wananchi."


"Kamati itakayoundwa kuisimamia idara ya usalama wa Taifa (TISS) ifuatilie pia matumizi ya fedha ya idara ya usalama wa Taifa kupitia fungu la 20 ndani ya mafungu ya serikali. Fungu hili huwa halikaguliwi na CAG ilihali JWTZ wenyewe hukaguliwa matumizi yao ya fedha.


"Marekani ukishakuwa mgombea Urais unalindwa na idara ya Secret Service ambayo ni idara inayojitegemea ikiwa tofauti na shirika la Ujasusi (CIA). Kama nasi tunataka Viongozi na Wagombea urais walindwe na usalama wa Taifa basi tuwe na idara maalum itakayokuwa huru.


"Sisi mambo yote ya usalama tumeyaweka ndani ya idara moja kiasi kwamba TISS inatumika sana kisiasa na CCM. TISS wanasahau kushughulika na mambo makubwa ya kiuchumi, ufisadi na uwekezaji wa nje na ndani, wanaanza kuhangaika na wanasiasa - wameenda wapi,wanafanya nini.


"Mapendekezo yetu ACT tuwe na idara inayojitegemea kufuatilia maslahi ya nchi na uwekezaji wa nchi. Iundwe idara maalum ya Tiss kufuatilia mambo ya nje ya nchi na kujua wenzetu wanafanya nini huko vyenye athari kwenye mipango na mikakati yetu ya ndani.


"Tunamuomba sana Mh. Rais Samia Suluhu aondoe hati ya dharura kwenye muswada wa sheria ya usalama wa Taifa, muswada uingie kwa utaratibu wa kawaida ili tupate sheria iliyo bora kwa wananchi na sheria bora kwa maafisa wa usalama wa Taifa."


Comments

News