RAIS DR. SAMIA NA UMUHIMU WA MARIDHIANO NA DEMOKRASIA KWA MAENDELEO ENDELEVU YA NCHI YETU.

RAIS SAMIA SULUHU HASSAN NI MUUMINI WA FALSAFA YA MARIDHIANO NA DEMOKRASIA KWA MAENDELEO ENDELEVU YA NCHI YETU.



Maridhiano ni hatua inayofikiwa kwa dhana ya kuleta makubaliano ya pamoja kwajambo lenye masilahi  kwa makundi  mawili   au  zaidi yenye mtazamo au itikadi tofauti katika nchi husika.


Inapotokea makundi haya hayakubaliani katika mizingira  baadhi ya mambo,   basi kwa taifa lenye  wastaarabu  wanakubalina   kukutana meza moja   kuzungumza namna   ya kwenda ili   kujikwamua katika   hali yakutoelewana na mambo haya huwa ni muhimu sana kufanyika wakati wa amani.


Inapobainika kama kuna jambo la namna hiyo kwa pande zote au upande mmoja basi kundi   moja huleta hoja ya   Maridhiano kwa   lengo la kutimiza   MALENGO Mahususi yaliyotarajiwa kwa Makundi yote Mawili na kuona kuna   umuhimu wakukaa pamoja ili kuzungumza. 


Mwaka 2007 nchi ya Kenya ilipitia katika wakati Mgumu sana katika mchakato mzima wa Uchaguzi Mkuu, jambo ambalo lilifanya kuzaliwa kwa Maridhiano ya kitaifa kwa kuyakutanisha Makundi yote kinzani.


Maridhiano hayo ya kawa ni baada ya kutokea mauaji ya baadhi ya watu nakufanya nchi hiyo kupoteza nguvu kazi ya taifa kutokana na zoezi zima la uchaguzi mkuu huo kutawaliwa na sintofahamu na kufanya uwepo wa vurugu nakusababisha viongozi wa kitaifa kupelekwa katika mahakama za kimataifa, kwa lengo la utetezi wa haki za binadamu. 


Nchini kwetu Tanzania suala la Maridhiano Imejitokeza katika vipindi mbalmbali vilivyopita na mpaka sasa RAIS WETU Ameendelea kujenga Msingi Uliyojengwa na Waasisi wa Taifa Letu. 


Sote tunajua Uundwaaji wa Serikali ya Umoja wa kitaifa katika Serikali ya Zanzibar ni matokeo ya Maridhiano hayo ambayo yalitokana namnyukano wa kisiasa kati ya chama tawala na vyama vya upinzani wakati huo chama chenye nguvu Tanzania Zanzibar kikiwa ni chama cha wananchi CUF. 


Nidhahiri Maridhiano yana nguvu kubwa duniani, kwani ukitazama kwa mawanda mapana   kwa sasa namna   siasa za Zanzibar   zinavyoleta   na   kuliweka taifa   hilo pamoja, kujenga   Mshikamano,   Upendo na Umoja   wa kitaifa kwa Wazanzibar


inafanya nchi hiyo kuwa na utulivu mkubwa na kufanya upatikanaji wa Maendeleo ya haraka katika nchi. 


Maamuzi ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kufanya Maridhiano ya kitaifa na kudumisha Uwepo wa demokrasia Inabainisha Mambo ya Msingi yafuatayo: -  

Mosi, Uzalendo wa   kiongozi Mkuu wa nchi, unafanya  uwepo   wa Maridhiano jambo ambalo linaongozwa na Dhamira Njema kwa kiongozi huyo KONGOLE Mheshimiwa Rais Wetu.


Pili, Nidhahiri kuwa Utashi wa kisiasa wa kiongozi wa Mkuu wa nchi huchochea uwepo wa Maridhiano katika Taifa husika jambo ambalo huleta Umoja wa kitaifa na katika hili KONGOLE  Mheshimiwa Rais Wetu kwani umeonyesha Upendo Mkubwa kwa Taifa lako.


Tatu, Maridhiano na Demokrasia ni Matoke, ya Uimara wa Uongozi wa chama kinacho Tawala Taifa Letu (CCM), kwani Umethibitisha Ukongwe Wake, kwa kuridhia kujengwa Maridhiano ya kitaifa na Udumishaji wa demokrasia ya Kweli, nidhahiri sote tunajua katika Bara la Afrika vipo Vyama Vya Siasa vimefanya kazi kubwa ya harakati za uhuru na ukombozi katika nchi zetu za Afrika hasa kusini mwa Afrika, lakini leo vimepotea yote haya ni Udhaifu mkubwa wa kukosa   uimara katika kujenga Maridhiano katika nchi zao KONGOLE Mheshimiwa Mwenyekiti wa CCM Taifa na Chama Tawala kwa Hatua hii kubwa ya kujenga Taifa Letu katika Msingi mzuri wa kidemokrasia na Maridhiano kwa Masilahi Mapana ya Taifa Letu. 


Sote ni Mashuhuda kwa Nchi zilizokosa fursa ya Maridhiano ya kitaifa, Tazama  KANU nchini Kenya na nchi nyinginezo, tazama Nchi ya Libya ambayo pia  ilikumbwa na athari  ya kukosekana kwa  uimara  wachama tawala hadi sasa taifa hili lipo kwenye mateso makubwa ya janga la vita yawenyewe kwa wenyewe.


Sote tunakubaliana kuwa Uimarishaji wa demokrasia na Maridhiano katika Taifa lolote inaleta matokeo chanya katika Maendeleo, Uimarishaji wa Uchumi wake wa ndani, kujenga twasira nzuri ya Taifa katika anga za kimataifa jambo hili huleta na kuimarisha diplomasia za kimataifa pia *KONGOLE* Mheshimiwa Rais Wetu kwa Hatua ya Maridhiano ya kitaifa na kudumisha demokrasia kwa Watu Wako. 


Mambo ya Msingi ya kuzingatiwa na Vyama vya Siasa hasa Vyama vya  Upinzani Ikiwemo Chama kikuu Cha Upinzani  Nchini CHADEMA.


Mosi, Ni vema Vyama   vyote vya siasa   kuunga na   kukubaliana na   jitihada na Dhamira Njema ya *RAIS WETU* ya kuanzishwa kwa Maridhiano na Uwepo wa  demokrasia kama taifa Pamoja na Uwepo wa Ukinzani wa kisiasa kwani kwa kufanya hivyo nchi itaimarika zaidi nakutunza Utaifa wake. 


Pili Vyama Vya Siasa vibebe Uzalendo Mkubwa kwa Taifa letu na kuachana namasilahi binafsi ya Vyama vyao ili RAIS WETU aweze kutimiza ndoto yake ya kujenga Nchi yenye Maendeleo Imara zaidi. 


Tatu, Vyama vya siasa vina wajibika kutunza Amani yetu kwa   kila   kimojawapo kuheshimu dhamira Njema ya Rais Wetu ya kuleta Maridhiano katika Nchi, kwani kwa kufanya hivyo itakua na tija kwa maendeleo ya taifa letu. 


Nne, Maridhiano na Demokrasia iweze kuwa dira ya kujenga Umoja na Mshikamano Wetu Kama Taifa, kadhalika ndani na nje ya Vyama vyetu vya Siasa.

 

Tano, uwepo wa   Maridhiano na kudumisha Demokrasia katika   nchi utasaidia   taifa   kupanga na kufikia Malengo yake mahususi ya kuleta maendeleo kwa watu wake hasa katika nyanja mbalimbali   kama vile masuala   ya kiuchumi na   shughuli zingine za   kijamii.


Nidhahiri kuwa Rais wetu Samia Suluhu Hassan ameamua kujenga Taifa imara lenye upendo, Mshikamano, Umoja, Amani na Utulivu kwa watu wake KONGOLE Mheshimiwa Rais Wetu. 


Sote tunakila sababu ya kukubali kwa dhamira Njema  Maridhiano na kudumisha demokrasia kwa afya ya Taifa letu, tuipende nchi yetu kuliko tofauti za vyama vyetu vya siasa kwani nchi ni zaidi ya vyama.


 Dhamira Njema ya RAIS WETU ni kuleta siasa safi na yenye tija kwa maendeleo ya nchi, hivyo Watanzania wote tuna kila sababu ya kukubali Maridhiano na Demokrasia ya Kweli ili tuweze kufanya maendeleo endelevu kwa pamoja.


"Uimara wa Vyama Vya Upinzani ni Uimara wa Chama Tawala katika Nchi yeyote, na Udhaifu wa Vyama Vya Upinzani kwa Taifa lolote ni Udhaifu wa Chama Tawala katika Taifa Hilo."


KONGOLE Mheshimiwa Rais Wetu kwa Uzalendo na Maamuzi Makubwa uliyofikia kwa kudumisha demokrasia ya Kweli na kufanya Nchi Yetu kujenga katika Falsa ya Maridhiano.


Sote Kama Taifa tuna Wajibu kubwa ya kuungana na Rais Wetu katika kujenga Taifa lenye Umoja na Mshikamano, kujenga Taifa lenye Upendo na Uzalendo wa kweli kwa kila Mmoja Wetu, kujenga Taifa lenye Nguvu katika Maendeleo yake na sivinginevyo, na kujenga Taifa lenye Amani na Utulivu kwa Watu Wake Wote.

Comments

News