MWENGE WA UHURU ULIPOTOKEA

Ipo siri kubwa kuhusu Mwenge wa Uhuru ambao hukimbizwa nchi nzima ,wapo wanaodhani kwamba aliyeleta Mwenge ni Rais wa kwanza wa Tanzania Mwl Nyerere ,hata baada ya Hayati Rais Magufuli kufuta baadhi ya sherehe na matukio yanayotumia gharama nyingi nchini, wapo tuliofikiria angefuta na mbio za Mwenge zinazotumia mapesa mengi.


Mwl Nyerere sio mwanzilishi wa mwenge wa Uhuru,  kwamba Mvumbuzi wa Wazo la kuwa na Mwenge wa Uhuru ni FOROJO GANZE, ambaye alikuwa ni mmoja kati ya wazee waliotumwa kufanya zindiko la nchi baada ya Uhuru mjini Bagamoyo mkoani Pwani. FOROJO GANZE, aliyezaliwa mwaka 1902, alifuatana na wazee hao na miaka yao ya kuzaliwa kwenye mabano nao ni;


1. Mzee Ramadhani (1920)

2. Ally Taraza (1920)

3. Komwe wa Kombe (1918)

4. Sheikh Yahya Hussein (1925)


Wazee hao walipewa kazi hiyo na wazee wa Mkoa wa  Dar es salaam enzi hizo kuhakikisha raia aliye madarakani hapingwi na mtu yeyote ,zindiko hilo lilifanyika Bagamoyo katika moja ya mashimo yanayopatikana wilayani hapo na baadae mwalimu Nyerere alipelekwa bagamoyo ,akachinjwa mbuzi na Nyerere akaambiwa atambike( aruke damu) baada ya kutokula kutwa nzima ( alifunga) jambo ambalo aliwahi kukiri kwenye moja ya mikutano yake.


 Hata hivyo katika mashimo yale FOROJO GANZE ndiye mtu pekee aliyeingia katika moja ya mashimo kwaajili ya kuuliza mizimu na aliwaacha wazee wenzake nje wakingoja ili kujua atakuja na jibu gani ili wakampatie Rais na wazee wa Dar es salaam.


Utamaduni wa Rais kuongea na wazee wa Dar es salaam unaendelea hadi sasa na wamekuwa na maamuzi ya kitaifa na husikilizwa sana wanachokisema, zindiko la bagamoyo linafanya kazi, 


Kilichoshangaza, mtu huyo FOROJO GANZE alipoingia shimoni alikaa siku kumi na siku ya kumi na moja alipotoka alikuwa hoi hajiwezi akiwa kama mtu aliyepigwa , na alikuwa akiongea lugha isiyojulikana.


" Tulimchukua akiwa hoi hadi Ikulu Dar es salaam na tulimfikisha mbele ya Mwl Nyerere na akatamka maneno yanayotumika au yanayohusu Mwenge wa Uhuru kwa kiswahili kisha akanyoosha juu mkono wake wa kulia ambao tayari ulikuwa umeandikwa namba 115, kisha akakata roho mbele ya Nyerere".alisema sheikh Yahya Hussein.


FOROJO GANZE alimwambia Nyerere " baba, sisi tunataka kuwasha Mwenge na kuuweka juu ya mlima Kilimanjaro, umulike hata nje ya mipaka yetu, ulete tumaini mahali pasipo na tumaini ,faraja palipo na huzuni, tumaini pasipo na tumaini ,Upendo penye chuki na heshima palipo na dharau".


" Baada ya kutamka hayo mbele ya Mwl Nyerere GANZE alikata roho na siku chache baadae mwalimu Nyerere akafanyia kazi maneno yake na kuanzisha Mwenge wa Uhuru ambao ulipandishwa mlima Kilimanjaro na Kapteni Alexander Nyirenda, aliyekuwa Jeshi la wananchi wa Tanzania ( JWTZ).


Kilichowashangaza wengi ni maneno yaliyoongoza yasemayo ;"UMULIKE NJE YA MIPAKA YETU ULETE TUMAINI " Ina maana ndani ya nchi kubaki gizani? aliuliza sheikh Yahya Hussein.


Pia sheikh Yahya ,alisema anashangazwa kwa nini FOROJO GANZE hakutangazwa kama mwanzilishi wa mwenge wa Uhuru? Kwani Baada ya mazishi ya FOROJO GANZE, ulianzishwa mwenge ambao ulikimbizwa nchi nzima mara tu baada ya Uhuru mwaka 1961 na unaendelea kukimbizwa hadi sasa.


Nyerere alimuagiza sheikh Yahya Hussein atafsiri maana ya ile namba 115 aliyokuwa ameiandika mkononi FOROJO GANZE, akamwambia; " namba 115 maana yake utakufa ukiwa na umri wa miaka 77 na taifa la Tanzania kwa kipindi hicho litakuwa na umri wa miaka 38 ya Uhuru na 77+38= 115, namba aliyoiandika FOROJO GANZE mkononi. 

Comments

Post a Comment

News