LILE SAKATA LA KEMIKALI ZINAZODAIWA KUWA NA SUMU MTO MARA TUME YA UCHUNGUZI YAUNDWA WADAU WATOA ANGALIZO KWA TUME KUFANYA KAZI KWA UWELEDI NA KUJA NA MAJIBU SAHIHI KWA MUSTAKABALI MPANA WA AFYA NA USALAMA WA BINADAMU NA VIUMBE HAI WENGINE.

 

Lile sakata la kudaiwa kuwepo kwa Kemikali za sumu katika mto Mara iliyowasilishwa Bungeni juzi na Mbunge wa Jimbo la Rorya Jafari Chege,Waziri Jaffo afika Mto Mara na kushuhudia hali halisi harufu kali,maji kubadilika rangi na vifo vya samaki.



Awali alipowasilisha hoja yake Bungeni Mbunge huyo alisema

    Namnukuu Mbunge wa Rorya

"Iundwe tume huru ambayo itatoa ukweli bila kuegemea upande wowote, hao watu wa NEMC na ofisi ya Bonde wanakuwepo kwemye maeneo hayo mara kwa mara, tunataka tume huru kufanya uchunguzi,”

Aidha, Mbunge huyo kijana alieleza kushangazwa na ukimya wa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu ya Rais (Muungano na Mazingira) tangu kutokea kwa tukio hilo ambalo limezua hofu na taharuki kwa maelfu ya wananchi katika vijiji vilivyo jirani na mto Mara.

Namnukuu Mbunge wa Rorya

“Waziri Jafo [Selemani Jafo] yuko kimya, ni wakati sasa kwa waziri huyu kijitokeza na kueleza umma wa Watanzania nini kinaenedelea mto Mara," amesema.

Katika hatua nyingine, Mbunge Chege alimuomba Waziri wa Maji, Jumaa Aweso kuangalia uwezekano wa kusaidia wananchi ambao wamezuiwa kutumia maji ya mto Mara kupata huduma ya maji hata kwa kuboresha visima vilivyopo.

Namnukuu Mbunge wa Rorya

"Leo ni siku ya tano, wananchi hawana huduma ya maji, Wizara ya Maji itoe fedha kugharimia uboreshaji wa visima vilivyopo na kuchimba vingine, maji ni uhai," Chege amesisitiza.

Baada ya kadhia hiyo Mkurugenzi wa NEMC, Dkt Samuel Gwamaka alikaririwa na vyombo vya habari akisema tume imeundwa kuchunguza chanzo cha uchafuzi huo ambao haujawahi kushuhudiwa katika mto huo unaotiririsha maji Ziwa Victoria.Uchimbaji wa madini unatajwa kuwa moja ya tishio la uhai wa mto Mara ambao ni muhimu kwa ustawi wa maisha ya maefu ya wananchi na ikolojia ya Serengeti.

HATIMAYE LEO 12.3.2022 SERIKALI YAINGILIA KATI SAKATA HILO.

Serikali imetangaza kuunda timu maalum itakayochunguza chanzo cha mabadiliko katika mto Mara yaliyopelekea maji kubadilika kuwa meusi huku viumbe hai wakiwepo samaki kufa.

Akizungumza baada ya kufika katika mto huo kujionea hali halisi leo Jumamosi Machi 12, 2022, Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Suleiman Jaffo amesema kuwa timu hiyo ya ataiunda leo ili ianze kufanya kazi mara moja.

Namnukuu Waziri Jaffo

"Nimejionea mwenyewe hali si shwari hapa kwa sababu harufu iliyopo hapa sio ile ninayoikuta kila nikija Mara kwa hiyo lazima Serikali ifanye jambo tena kwa haraka ili tupate majawabu nini chanzo na kipi kifanyike kabla watu hawajaathirika," amesema Jafo. 

Amesema kuwa katika timu hiyo anayokwenda kuunda hivi punde kutakuwepo na wataalam mbalimbali wakiwepo wataalam wa miamba na kemikali ambao watatakiwa kujua kama mabadiliko hayo yamesababishwa na kemikali au miamba.

Awali, Mkurugenzi wa Uzingatiaji na Utekelezaji wa Sheria wa Baraza la Taifa la Mazingira (Nemc), Redempta Samuel amesema kuwa timu ya wataalam ilifika katika eneo la mto huo tangu Machi 10, 2022 kwa ajili ya kufanya uchunguzi.

Amesema kuwa hadi sasa wamekwishachukua sampuli 32 kutoka katika maeneo mbalimbali ya mto huo sambamba na ziwa Victoria na kwamba uchunguzi unaendelea kujua tatizo ni nini.

Katika hatua nyingine waziri Jaffo ameshindwa kuingia ndani ya mto huo kama ilivyokuwa imepangwa awali baada ya eneo la mto katika upande wa pili wa daraja la Kirumi kuzingirwa na kujaa magugu maji yaliyofika katika eneo hilo muda mfupi baada ya waziri kuwasili katika eneo hilo.



Comments

News