Kiongozi wa upinzani nchini Tanzania Freeman Mbowe amekutana na rais Samia Suluhu Hassan Ikulu jijini Dar es Salaam, baada ya kuachiwa huru kufuatia yeye na wenzake watatu kufutiwa mashtaka ya uhujumu uchumi na ugaidi siku ya Ijumaa jijini Dar es salaam.

 


“ Kitu kikubwa tulichojadiliana ni kuwa, Tanzania ni  yetu sote na tunapaswa kufanya kazi pamoja, kuijenga, lakini hili linawezekana tu iwapo tutajenga uaminifu na kudai haki, pamoja na kuheshimiana. Hii itatusaidia kupata nafasi ya kuijenga nchi yetu, alisema rais Samia.

“Tumekubaliana kuwa, njia nzuri ya kuwa na maridhiano ni wakati kuna haki.Tumepitia madhila mengi, hakuna haja ya kuyarudisha mara kwa mara, badala yake tunapaswa kusonga mbele na kuwa na siasa safi na kuiunga mkono serikali, na tunatumai kuwa itatuunga mkono kwenye shughuli zetu ili kila mtu afurahi, “ alisema Mbowe

Mbowe alikuwa gerezani tangu Julai mwaka 2021 alipokamatwa  mjini Mwanza wakati akijiandaa kuhotubia kongamano la kudai kuwepo kwa Katiba mpya nchini humo.

Hatua hii imepongezwa na wadau mbalimbali nchini humo na kuelezwa kama jitihada za rais Samia kutaka mshikamo wa kitaifa, baada pia ya kukutana na mwanasiasa mwingine wa upinzani Tundu Lissu jijini Brussel nchini Ubelgiji mwezi Februari.

BONYEZA LINK KUTAZAMA VIDEO

Comments

News