BUSARA ZA ROMAN,MO NA GSM WAJIFUNZEHAPA JUU YA MUSTAKABALI MPANA WA VIGOGO WA KARIAKOO
Bilionea ambaye ni Mmiliki wa Club ya
Chelsea ya England Roman Abramovich
amethibitisha kuwa anataka kuiuza club hiyo
ambapo anafanya hivi kwa maslahi mapana
ya Club, Wadhamini na Wafanyakazi wa Club.
Ningependa kutoa taarifa kuhusiana na
tetesi zinazoendelea kwenye vyombo vya
habari kuhusiana na umiliki wangu Chelsea,
siku zote nimekuwa nikifanya maamuzi kwa
sababu ya maslahi ya club, kwa hali
inavyoendelea sasa nimeamua kuiuza club"
Roman Abromavich.
--
Roman aliinunua club hiyo 2003 kwa pound
milioni 140 (Tsh Bilioni 433) na sasa
ameamua kuiuza baada ya vita ya Ukraine
kuisababishia Russia na Wawekezaji wake
kuwekewa vikwazo au biashara zao
kusitishwa sehemu mbalimbali.
Kwa mujibu wa Forbes Chelsea sasa ina
thamani ya pound Bilioni 2.4 (Tsh Trilioni
7.4).
Roman katika taarifa iliyotolewa na Chelsea
anasema atauza club hiyo na pesa zote
alizouza zitaenda katika mfuko maalum wa
kusaidia Waathirika wa vita nchini Ukraine na
wala hana lengo la kujipatia faida.






Comments
Post a Comment