HAKUNA FARU MWEUSI RUFIJI.

 

Wizara ya Maliasili na Utalii imetoa ufafanuzi

kuhusu taarifa iliyotolewa na mtandao wa

Tanzania Times tarehe 3 Machi, 2022

ikieleza kuonekana kwa faru mweusi katika

Hifadhi ya Taifa Nyerere "Taarifa hiyo

ambayo inaendelea kusambaa katika vyombo

mbalimbali vya habari na mitandao ya kijamii

sio sahihi na tunaomba ipuuzwe"

"Ukweli ni kwamba hakuna Faru mweusi

aliyeonekana katika hifadhi ya Taifa ya

Nyerere kama ilivyoripotiwa na mtandao huo"

"Wizara inasisitiza kuwa Msemaji Mkuu wa

masuala ya wanyampori hapa nchni ikiwemo

utoaji wa takwimu na taarifa za wanyamapori

kwa umma ni Wizara ya Maliasili na Utalii na sivinginevyo"



KARIBU NYERERE NATIONAL PARK RUFIJI.

https://www.google.com/search?q=nyerere+national+park+Rufiji&client














Comments

News