Semina ya TAKUSKA WILAYA YA RUFIJI MUWAKILISHI WA DC AFISA ELIMU TAMADUNI ASIMAMIA SHOW VYEMA
Leo Februari 23. 2022 imetaranyika semina yamwongozo wa kuzuia na
kupambana na Rushwa kwa Vijana wa Skauti
mashuleni na Vyuoni katika Ukumbi wa chuo
Cha maendeleo ya WaNananchi (FDC) IkwiririWilayani Rufiji.
Mafunzo hayo yalihudhuriwa na Kamanda wa
TAKUKURU Wilaya, Kamanda wa TAKUKURU
Ikwiriri, Maafisa toka idara ya Elimu Msingi
na Sekondari, Maafisa elimu kata, Wakuu wa
Shule, Walimu wakuu pamoja na Kamati
tendaji ya Skauti ngazi ya Wilaya.
wa Wilaya ya Rufiji, Afisa Elimu Taaluma
Wilaya ya Rufiji Tunsume Mwakipesile
alisema Utekelezaji wa Mwong0zo huo
utawawezesha Vijana wa skauti kuwa
wawajibikaji, wazalendo na kujenga Jamii
itakayoichukia Rushwa.
Kwa upande wake Kaimu Afisa Elimu
ambaye pia ni Afisa Elimu Vifaa na Takwimu
Sekondari Geoffrey Mwakagali amewataka
Walimu Wakuu na Wakuu wa shule
kuhakikisha wanaanzisha na kuhuisha klabu
za wapinga Rushwa mashuleni na kuwataka
kuzungumza suala la mapambano dhidi ya
Rushwa Kama ajenda katika vikao vya
wazazi.
Kwa upande wake Kamishna wa skauti
Wilaya ya Rufiji Latifa Lukwaro ametoa shukrani kwa Mkuu wa Wilayà ya Rufiji
ambaye pia ni Mlezi wa Chama Cha Skauti
Wilaya, pamoja na Mkurugenzi mtendaji wa
Halmashauri kupÃtia Maafisa elimu Msingi na
Sekondari kwa kutoa ushirikiano na
kuwezesha Shughuli za Vijana wa skauti
shuleni.
Emmanuel Kapandila
(Cc) Rufiji Dc.






Comments
Post a Comment