MADAWATI 576 KUBORESHA MIUNDOMBINU YA ELIMU
Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Meja Edward
Gowele amekabidhi madawati 100 kwa
Mwalimu Mkuu shule ya Msingi Kilimani na
kumtaka kuyatunza madawati hayo ili
yaendelee kutoa ari ya usomaji kwa
wanafunzi
Awali, akitoa taarifa fupi ya uboreshaji wa
miundombinu ya shule za msingi kwa niaba
ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri,
Afisa Elimu Msingi Wilaya ya Rufiji Edward
Buganga amesema, Halmashauri ya Wilaya
ya Rufiji Imetoa jumla ya shilingi Milioni 34.6
mapato ya ndani kutengeneza madawati 576
ambapo kati ya madawati hayo madawati
100 yamekamilika na mengine yakiwa katika
hatua ya ukamilishaji huku tenda zikiwa
zimetolewa kwa vikundi mbalimbali vya
mafundi wilayani humo.
Aidha Mhe. Gowele ametoa shukrani kwa
mdau wa elimu ambaye amejitolea usafiri
kusafirisha madawati hayo toka ikwiriri hadi
shuleni na kutoa wito kwa wadau wengine
wa maendeleo kuendelea kushirikiana na
jamii za wanarufiji kuchangia katika shughu
za maendeleo.






Comments
Post a Comment