Kituo cha Huduma za Pamoja Mkoani Pwani chamkosha Mhe. Bashungwa Awataka Wakuu wa Mikoa kuiga mfano wa Pwani.
OR-TAMISEMI
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais ofisi,
TAMISEMI Mhe. Innocent Bashungwa
amefurahishwa na Kituo cha Huduma za
Pamoja ( One Stop Center) kilichoanzishwa
kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
kwa ajili ya kutoa huduma za haraka kwa
Wananchi wa Mkoa huo.
Akizungumza akiwa ziarani Mkoani Pwani
Mhe. Bashungwa amesema uwepo Huduma
muhimu sehemu moja inamrahisishia
mwananchi kutohangaika kuzunguka mji
mzima kutafuta Ofisi mbalimbali za kutatua
shida zake.
Katika kituo hiki tunaona huduma
mbalimbali zinapatikana katika eneo moja
hapa tunawaona TRA, Uhamiaji, DAWASA,
Magereza,TANROAD,TARURA, NEMC,
TANESCO na wengine wengi sasa
mwananchi wetu wanaweza kunaliza shida
zao sehemu moja na sio ile mtu anafunga
safari mpaka Ofisi flani kisha unaambiwa
suala hili sio la hapa nenda Ofisi nyingine
inachosha lakini kwa hapa mahitaji mengi yawananchi yanatatuliwa sehemu moja,
alisema Bashungwa.
Sasa Niwatake Wakuu wa Mikoa yote nchini
kuiga mfano huu na kuanzisha One Stop
Center kwenye Ofisi zao ili wananchi wa
maeneo hayo waweze kupata huduma bora
kwa urahisi na sio kusumbuka kama zamani.
Kituo cha Huduma za Pamoja Mkoani Pwani
kimeanza takribani mwezi mmoja sasa na
kinajumuisha Taasisi zote Wezeshi kutoka
huduma katika eneo moja.






Comments
Post a Comment