MBUNGE ANASWA NA DAWA ZA KULEVYA



Mbunge wa zamani katika jimbo la Budalangi mjini Nairobi, Raphael Wanjala,mfanyabiashara wa kike, Joyce Akinyi na watu wengine watatu wamekamatwa katika eneo la Isinya nchini Kenya kwa tuhuma za kusafirisha dawa za kulevya.

Watuhumiwa hao watano walikamatwa juzi jioni wakiwa wamebeba kemikali bashirishi za dawa za kulevya ambazo zinadaiwa zilitoka nchini Tanzania.

Kwa mujibu wa mtandao wa redio Capital Fm ya nchini Kenya,ulibainisha jana kuwa,Mkuu wa Kikosi cha Polisi kinachopambana na dawa za kulevya,Hamisi Masa alisema  watuhumiwa hao watano wanashikiliwa kwa uchunguzi zaidi.

‘”Tumewakamata na kemikali bashirishi ambazo tunaamini ni dawa za kulevya. Kemikali hizo zimepelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi ili tuweze kujua ukweli, kabala ya hatua zaidi kuchukuliwa,”alisema Masa.

Comments

News