Dc Sawala apewa U RC Mabadiliko madogo ya Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko madogo ya Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mabasi Yaendayo Haraka (UDART). Miongoni mwa watu hao ni Patrick Sawala aliyewahi kuwa Mkuu wa Wilaya Rufiji na Tandahimba ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa Mtwara na Daniel Chongolo aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Songwe na Waziri Kindamba aliyeteuliwa kuwa mkurugenzi mkuu wa UDART. Kwa Mkeka kamilia fungua kiungo hapa chini Mabadiliko Madogo Serikalini




